ads

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameitwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Boaz.


Lowassa akizungumza na Mwananchi jana (Jumatatu), amesema ameitwa kwa DCI lakini hajui anachoitiwa.

Hata hivyo, amesema anahisi ni kauli yake kuhusu mashehe wa kikundi cha Uamsho cha Zanzibar wanaoshtakiwa kwa tuhuma ya ugaidi.

 “Ni kweli nimetakiwa niripoti kesho(leo) saa 4:00 asubuhi katika ofisi ya DCI. Sijui wananiitia nini, lakini nahisi ni kuhusu nilichosema kuhusu mashehe wa Uamsho,” amesema Lowassa.

Jana katika taarifa kwa vyombo vya habari, Lowassa alikaririwa akimtaka Rais John Magufuli kuwaachia huru mashehe hao wanaoshikiliwa kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Taarifa hiyo ilisema Lowassa alitoa ombi hilo alipozungumza katika futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara.

Credit - Mwananchi
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: