Katibu Mkuu wa Chama Dkt. Vincent Mashinji, Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambe ambaye pia ni Mkiti wa Chama Kanda ya Kusini pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Zubeda Sakuru wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Mbamba Bay. Wamepelekwa kituoni kuhojiwa ambapo Katibu Mkuu Dkt.
Mashinji ametakiwa kueleza kwanini yuko Mbamba Bay na aeleze amekwenda kufanya nini.
Polisi wamemkamata Katibu Mkuu Dkt. Mashinji, Mbunge Mwambe na Mbunge Zubeda baada ya kuvamia kikao cha ndani kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu Dkt. Mashinji kukagua shughuli za chama katika majimbo ya kanda hiyo iliyoanza leo.
Tutaendelea kuwajuza.
Tumaini Makene
Post A Comment: