Msanii wa Bongo Fleva, Peter Msechu amesema kutokana na muziki wake kwa sasa kuhitaji mchango wa watu wengi ili kuwa bora zaidi amelazimika kutoa fursa kwa mashabiki wake kumuandikia nyimbo na kununua.
Mwimbaji huyo ameeleza kuwa mtu yeyote mwenye wimbo mkali amtafute na wakae chini kuongea kwa ajili ya kupatana bei, lakini kiasi cha fedha unachoweza kupata kinaweza kufika hadi sh. milioni moja.
“Kuna mtu amenicharge juzi wimbo moja sh. milioni moja na ni wimbo mkubwa sana, ninafikiri ndio wimbo utakaofuata baada ya Ramadhan,” Msechu amekiambia kipindi cha Ladha 3600 cha E Fm.
“Kuna mdada mmoja anakaa Arusha ameniandikia nyimbo mbili aiseee!!, nilitengemea hata atanidai milioni tano au sita lakini alikataa kabisa akaniambia kwa heshima yako wewe ziimbe tu, unaona kabisa wapo watu wenye vipaji hivyo lakini wamejificha,” ameongeza.
Msechu ameongeza kuwa toka awali alishaweka wazi kuwa yeye hajui kuandika nyimbo hivyo watu wasishangae kwani anafanya hivyo ili kuepuka kukurupuka kutoa nyimbo kama ilivyokuwa awali ila sasa hivi anajaribu kujipa muda.
Post A Comment: