Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga SC, Juma Mwambusi amefunguka na kuitetea klabu yake baada ya kichapo cha goli 4-2 dhidi ya AFC Leopards kutoka Kenya na kutupwa nje ya michuano ya SportPesa Super Cup kwa kusema timu yake imekosa muda wa maandalizi.
Juma Mwambusi ambaye kwenye michuano ya Supersport Super Cup amechukua nafasi ya Kocha mkuu Lwandamina aliyelikizo amesema Klabu ya Yanga imetolewa kwa kukosa muda wa maandalizi kwani michuano hiyo haikuwa na muda mrefu wa kuruhusu vilabu kujiandaa.
“Tumetolewa kweli michuano ilikuwa ni migumu kwetu hatukuwa na muda wa kutosha wa maandalizi ya michuano hii muda ulikuwa mfupi sana, hii imetuathiri sana kwenye michezo yetu yote miwili”Amesema Mwambusi mapema baada ya mchezo kumalizika.
Klabu ya Yanga inakuwa timu ya nne kutolewa kwenye michuano hiyo yenye msisimko wa aina yake inayodhaminiwa na kampuni ya Kubashiri ya SportPesa, baada ya Simba,Singinda United na Jang’ombe Boys ya Zanzibar.
Post A Comment: