Aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), James Comey ameishtumu Ikulu ya Marekani kwa kumharibia jina na kusema uongo kuhusu shirika hilo.
Comey ambaye aliyefutwa kazi ghafla na Rais Donald Trump alisema hayo jana Alhamisi, baada ya kuanza kutoa ushahidi mbele ya maseneta nchini Marekani kuhusu tuhuma kwamba Urusi iliingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka uliopita.
Mkuu huyo wa zamani wa FBI amewaambia maseneta waliomhoji kuwa alikuwa na mazungmzo ya siri na Rais Trump. Aidha, ameshtumu matamshi ya Ikulu ya Marekani kuwa FBI ilikosa imani naye.
Trump alimfuta kazi Comey Mei 9, mwaka huu baada ya FBI kutangaza kuchunguza madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani, madai ambayo Urusi imekanusha.
Comey amesema, Trump alimwambia asitishe mchakato wa FBI kumchunguza Michael Flynn, aliyekuwa mshauri wake wa masuala ya usalama wa Taifa kwa madai kuwa alikuwa na mawasiliano ya karibu na maofisa wa Urusi kipindi cha uchaguzi.
Post A Comment: