ads

Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ametoa siku saba kwa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amuombe radhi kwa kosa la kumuweka ndani wakati alipokuwa anakabidhi rambirambi kwa wazazi waliofiwa kwenye ajali ya gari la Shule ya Msingi Lucky Vincent.


Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo Ijumaa, Lazaro amesema mpaka sasa ameshindwa kuelewa ni kwanini mkuu huyo aliagiza meya pamoja na wenzake wakiwemo viongozi wa dini, madiwani, wawakilishi waliotoa rambirambi na mwenye shule kukamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa ndani.

"Mimi sikuwa na shida na RC na kitendo cha kumuweka ndani kiongozi wa dini, paroko, kiongozi wa dini ya Kiislamu ni kitendo ambacho si cha kibinadamu na anapaswa aombe radhi umma,"amesema.

Pia, amemtaka kutafakari nafasi yake na kuona kuwa anafaa kuendelea kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha kwasababu ameonyesha kuwatumikia wananchi ambao hawaheshimu.

"Hana heshima na mbunge, madiwani, watu wenye degree zao, haheshimu viongozi wa dini halafu bado anataka uongozi,"amesema.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: