ads

KANISA la Anglikana Tanzania, limesema linaunga mkono jitihada kubwa za Rais Dk. John Magufuli kutetea rasilimali za taifa hasa kwenye sakata la kuzuia mchanga wenye dhahabu (makinikia) na kwamba linamtaka kukaza kamba zaidi ili kuwabana mafisadi na watumishi wa umma ambao wamesababisha taifa kufikia hapa lilipo.


Mbali na hilo, serikali imetakiwa kufanya marekebisho ya sheria zake ambazo hazina maslahi mapana kwa taifa, kanuni na sera za nchi.

“Haiwezekani kwa viongozi wa umma waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali za nchi kushindwa kujua iwapo kuna kampuni zinazofanya kazi za uchimbaji na usafirishaji wa mchanga wa madini zikiwa hazina usajili nchini na vitendo hivyo vinatokana na kushuka kwa maadili na hofu ya Mungu katika mioyo yao,” alisema Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu Jacob Chimeledya.

Askofu Chimeledya aliyasema hayo jana kwenye ibada ya kumsimika rasmi kwenye Dayosisi mpya ya Kanisa la Anglikana Biharamulo, Askofu Vitalis Yusuph, ambaye awali alikuwa katibu wa Dayosisi ya Kagera kabla ya kugawanywa.

Askofu Chimeledya alisema kanisa hilo linaunga mkono jitihada hizo za Rais Magufuli na kwamba hatua hiyo inalenga kuwarejeshea hadhi wananchi wa Tanzania ambao Mungu mwenyewe aliwapatia rasilimali nyingi ili ziwanufaishe, lakini wamekuwa wakitaabika na maisha kutokana na baadhi ya viongozi wa umma kukosa maadili na hofu ya Mungu.

Kadhalika, aliitaka serikali kurekebisha mikataba ya madini ambayo imeendelea kuifanya Tanzania kuwa “shamba la bibi” na kusababisha wananchi kuendelea kuwa maskini wa kutupwa.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: