ads

Usiku wa kuamkia jana Jumapili, bondia Francis Cheka alichezea mkong'oto kwenye pambano na Enes Zecirevic huko Uswisi.


Cheka alipigwa kwa pointi za majaji 3-0 kwenye pambano hilo la raundi nane la uzani mwepesi wa juu (kg 81) lililofanyika mjini Geneva.

"Nisingeweza kushinda kwa pointi, nilijua matokeo yale baada ya kumaliza raundi zote. Siku zote unapocheza ugenini na kumaliza raundi zote ni vigumu kupewa ushindi dhidi ya mwenyeji, ndivyo ilivyokuwa hata na kwangu.

"Nimeumizwa kuharibu rekodi yangu, lakini sijashangazwa na kupigwa kwa pointi kwani ni ushindi ambao yoyote anaweza kupewa," alisema Cheka
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: