ads

Familia ya beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England jana Jumamosi imetembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS kilichopo Mombasa, Unguja.


Sakho amefuatana na mke wake Madna na watoto wake wawili wa kike.

Sakho akiwa Zanzibar alizindua mashindano ya Coco Sports Ndondo Cup mchezo ambao Taifa ya Jang’ombe walifungwa 2-1 na Mlandege SC.

Sakho yupo  visiwani Zanzibar tangu  Juni 17, kwa ziara ya kiutalii. Awali ziara hiyo, alianzia Tanzania Bara kisha kurejea Ufaransa na baadaye kurudi Zanzibar
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: