KIONGOZI wa chama cha ACT–Wazalendo, Zitto
Kabwe, amemshauri Rais John Magufuli, kuwafikisha kwenye vyombo vya
nidhamu na sheria wote aliowatumbua tangu alipoingia madarakani.
Alisema watu hao waliotumbuliwa kuanzia mwaka jana hadi Agosti mwaka
huu, ambao idadi yao ni takribani 130, wafikishwe kwenye vyombo vya
kisheria na nidhamu ili viwaeleze Watanzania kuhusu kile wanachotuhumiwa
nacho watumishi hao.
Halikadhalika alimshauri Rais Magufuli kufuata misingi ya haki na
usawa katika kuwachukulia hatua baadhi ya watumishi wa umma
aliowatumbua kwa tuhuma mbalimbali.
Zitto aliyasema hayo jana Dar es Salaam katika mkutano mkuu wa
ACT-Wazalendo, unaojadili mambo kadhaa yakiwamo, hali ya siasa nchini
kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 pamoja na uzoefu wa kisiasa wa
mataifa mengine ya Afrika.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: