CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
kimeibua tena hoja iliyoonekana kupoa kwa muda mrefu ya mchakato wa
katiba mpya baada ya kuagiza vikao vyao vya ndani vianze kuifanyia kazi
kwa kuidai kuanzia ngazi ya msingi hadi taifa.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vicent Mashinji, alitoa agizo hilo
jana alipokuwa Mkuranga, Pwani wakati wa harambee ya kuchangisha fedha
za kumalizia ununuzi wa jengo ambalo litatumika kama ofisi ya wilaya ya
chama mkoani humo.
Akizungumza katika harambee hiyo, Dk. Mashinji alisema bado dai la
katiba iliyopendekezwa katika taifa ni muhimu kwa maslahi ya taifa.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: