Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amesema ni lazima uwapo uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu ya msingi.
Pinda
aliyasema hayo nyumbani kwa Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela wakati
wa harambee ya kuchangia uboreshaji wa Shule ya Canon Andrea Mwaka
inayomilikiwa na Kanisa la Anglikana.
“Tukikosea katika elimu ya msingi huko kwingine ni uongo, lazima tuwekeze kwenye elimu,” amesema.
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dk Jacob Chimeledya amesema shule hiyo
inayotoa elimu ya msingi hadi kidato cha nne, ilianzishwa mwaka 1950 kwa
ajili ya wamisionari waliokuja nchini kueneza dini na inapokea
wanafunzi wa dini zote.
“Shule
hii ina wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali. Kwa sababu ya ujio wa
makao makuu tunataka kuboresha uzio, maabara, majengo na taaluma kwa
kuongeza walimu kutoka ndani na nje wenye sifa za kufundisha kwenye
shule hii,” amesema Dk Chimeledya.
Ameisema
uboreshaji huo utagharimu Sh1 bilioni, lakini harambee zitakuwa kwa
awamu mbalimbali na wamepata ahadi na fedha taslimu Sh60 milioni huku
akiwaomba watu kuchangia.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: