Watu wengi wamekuwa wakipata shida kuhusu suala la uzito kupita kiasi na
kushindwa kutambua namna gani sahihi ya kukabiliana na tatizo hili.
Hapa ninazo njia kadhaa zitakazokusaidia kupunguza uzito wa mwili wako:-
Weka mbali vyakula na vinywaji visivyokuwa vya lazima
Ni vyema kuweka mbali vyakula visivyokuwa vya lazima yaani vile viburudisho kama vile soda na vingine vingi vyenye asili hiyo.
Kunywa maji mara kwa mara
Jenga utaratibu wa kunywa maji mara kwa mara hasa kabla ya kula zoezi hili huweza kusaidia kupunguza uzito mkubwa wa mwili endapo zoezi hilo litafanyika mara kwa mara.
Utulivu wakati wa kula
Unapokula hakikisha upo sehemu tulivu na huna shughuli nyingine zaidi ya kula tu, kwani baadhi ya watu hula huku wakiangali runinga au wakichezea simu au kopyuta. hali hii huweza kuchangia mhusika kula zaidi kuliko pale anapokula bila kuwa na shughuli nyingine.
Pata muda wa kutosha wa kulala
Hali ya kukosa usingizi wa kutosha huchangia kuharibu hamu ya chakula, na baadaye kuchangia kuvurugika kwa mpangilio wa mlo wako au ratiba ya kula na hivyo kujikuta ukiingia kwenye tatizo hilo la unene kupita kiasi hivyo ni vyema kupata muda wa kutosha wa kulala kwa faida zaidi.
Punguza matumizi ya vinywaji vyenye sukari
Vinywaji hivyo huchangia kuongezeka kwa tatizo hilo la uzito mkubwa hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vinywaji hivyo ili kupata matokeo mazuri zaidi.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: