Serikali imesema hakuna uhaba wa dawa nchini kwa sasa kama inavyoendelea
kuuenezwa na baadhi ya watu na kusisitiza kuwa habari hizo ni za
upotoshaji na zinalenga kuwatisha wananchi.
Kauli
hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akitolea
ufafanuzi ripoti mbalimbali ambazo zinatolewa na baadhi ya taasisi
zisizo za kiserikali zinazoonesha kuwepo kwa uhaba wa dawa na vifaa tiba
nchini.
Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo Mhe Mwalimu amesema ni kweli kulikuwa na uhaba wa chanjo zinazotolewa kwa watoto wadogo na siyo uhaba wa dawa zote kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu amesema wameanza kubaini vituo vya afya ambavyo vilikuwa na upungufu wa dawa na chanjo tayari kwa kupeleka dawa hizo kwa kuwa bohari ya dawa ina dawa za kutosha.

DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: