JUMUIYA ya Vijana ya Chama cha Wananchi
(Juvicuf), imesema haiungi mkono ziara ya kichama ya Profesa Ibrahim
Lipumba na wafuasi wake itakayofanyika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Imesema kuwa ziara hiyo itaongeza mpasuko ndani ya chama ikizingatiwa kwamba bado kuna mgogoro.
Mwenyekiti Juvicuf, Hamidu Bobali aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana mbele ya waandishi wa habari.
Alisema vijana wa jumuiya hiyo wasishiriki katika ziara hiyo kwa kuwa
hawamtambui Prof. Lipumba kama bado ni Mwenyekiti wa CUF, na pia si
mwanachama.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: