Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea fedha taslimu sh. milioni 25.62
pamoja na nguo zenye thamani ya sh. milioni mbili kutoka kwa wadau
mbalimbali.
Makabidhiano ya michango hiyo yamefanyika leo (Ijumaa, Oktoba 14,
2016) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es
Salaam.
Akiwashukuru wadau hao Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.
“Nawashukuru kwa kuamua kutumia siku ya leo ya kukumbuku ya kifo cha
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwachangia wenzetu
waliopatwa na maafa,” amesema.
Waziri Mkuu amesema michango hiyo ni muhimu na inaonyesha mshikamano wa dhati uliopo baina ya Watanzania.
Misaada hiyo imetolewa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) sh.
milioni 20, Mtandao wa Wasanii Tanzania sh. 620,000 na nguo mifuko
miwili, Chama cha Makatibu Mahsusi (TAPSEA) sh. milioni tano.
Wengine ni Umoja wa Wafanyabiashara Ndogondogo soko la Kariakoo ambao
wametoa marobota mawili ya nguo (suruali, kanzu na nguo za akinamama na
moja la wanasesere kwa ajili ya watoto waliopatwa na maafa vyote vikiwa
na thamani ya sh. milioni mbili.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: