Moja ya Jambo ambalo nimeona ni vema nikamkumbuka Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere siku ya leo Oktoba, 14 ni uwezo wake wa kuona mbali
hasa pale aliposhauri Uanzishwaji wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa
mwaka 1991 baada ya Tume ya Jaji Nyalali kuwasilisha maoni yake kwa
Rais Mwinyi.
Taifa letu linahitaji aina ya viongozi wenye uwezo wa kuona mbali zaidi, kuona kabla ya wengine na kuona sana kuliko wengine. Tangu awamu ya kwanza mpaka leo Taifa letu bado halijapata kiongozi mfano wa Nyerere katika kuona mbali, bado hatujapata!
Uongozi ni kuona mbali kuliko wengine. Pamoja na kuwa asilimia 80 ya waliohojiwa na Tume ya Jaji Nyalali hawakutaka mfumo wa vyama vingi vya siasa na asilimia 20 pekee ndio waliotaka, bado uamuzi ulifanyika kwa kuzingatia vision ya Mwalimu Nyerere kuwa Taifa letu sasa ni wakati muafaka tukaenda na Mfumo wa vyama vingi vya Siasa.
Leo hii, kila anayejigamba kumuenzi Mwalimu Nyerere na maneno yake na vitendo vyake vinaashiria ama kuzuia au kuminya Uhuru wa vyama vingi ni muongo na wala hawezi kutuminisha kuwa anamuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuwa vitendo na maneno yake vikakinzana na dira aliyotuachia Mwalimu Nyerere.
Tunaowajibu sisi kama viongozi kuzitafakari njia zetu ili kujenga msingi imara wa maendeleo ya Taifa letu. Taifa letu kwanza, mengine baadaye kwa kuwa Taifa letu ni kuu na kubwa kuliko matamanio yetu ya kuwa viongozi na kuzidi yote Taifa letu ni kuu kuzidi rangi ya bendera za vyama vyetu.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: