Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr), imesema kutokana na mbu wa malaria kujenga usugu wa dawa ya Pyrethroids kwa baadhi ya maeneo nchini, ugonjwa huo sasa umeanza kurudi kwa kasi hasa sehemu zilizofanyiwa utafiti na kugawa vyandarua.
Akizungumza
katika kongamano la 30 la Kimataifa la Wanasayansi Watafiti jijini Dar
es Salaam jana, Mtafiti katika Mradi wa Amani Medical uliopo chini ya
Nimr, Said Magogo alisema kufuatia tatizo hilo kituo hicho kipo kwenye
mchakato wa kuhakikisha kinapata dawa mbadala.
Alisema
mbu hao wanajenga usugu hata kwenye dawa ya kuua mazalia yao
inayotumiwa katika vyandarua, hivyo kuishi muda mrefu zaidi.
“Mfano
Korogwe ambako zimewekezwa nguvu nyingi hasa katika kugawa vyandarua
kwa asilimia 80, tunaendelea kuangalia dawa mbadala ambayo tutaitumia
kuangamiza mbu hao,” alisema.
Alisema
chanzo cha usugu ni aina hiyo ya dawa kutumika muda mrefu, hivyo hata
inapotokea mbu akataga mayai tayari yanakuwa na dawa hiyo si rahisi
kuuawa.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: