Waziri wa ardhi, nyumba na makazi Mh. William Lukuvi, amesema zaidi ya nyumba 35,000 zilizopo katika jiji la Mwanza hazina hati, jambo linalosababisha serikali kupoteza zaidi ya shilingi trilioni moja kwa mwaka kutokana na asilimia 88 ya nyumba kutolipiwa kodi katika maeneo mbalimbali nchini.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo jijini Mwanza wakati wa uhamasishaji
wa urasimishaji wa makazi holela, sambamba na utekelezaji wa mpango
kabambe wa miaka 10 wa jiji la Mwanza utakaowawezesha wananchi kupanga,
kupima na kumilikishwa ardhi na nyumba zao, huku akiagiza waliojenga
maeneo hatarishi kujiandaa kuondoka kabla serikali haijawafikia kwani
lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa kufikia juni 30 mwaka 2017 watu
wote wawe wamepimiwa maeneo yao na kupewa hati.
Aidha, waziri Lukuvi amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watu
wakiwemo maafisa ardhi kwenda mitaani kinyemela bila kupitia ofisi za
serikali hasa nyakati za usiku kwa lengo la kuwaonyesha viwanja
wananchi.
Kiomoni Kibamba ni mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mwanza,
anasema zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wa jiji la Mwanza wanaishi kwenye
makazi holela, hatua ambayo imeilazimu wizara ya ardhi, nyumba na
makazi kubuni mradi wa urasimishaji wa makazi holela, je nini matokeo ya
utekelezaji wa mradi huo.
Waziri Lukuvi ametangaza rasmi kwamba kuanzia sasa michoro ya
mipango miji itaanza kutolewa mwanza badala ya kupelekwa dar es salaam
kwa mikoa mitano ya kanda ya ziwa, ambapo amteua deo kalimenzi ambaye ni
afisa mipango miji wa jiji la mwanza kuwa mkurugenzi msaidizi wa
mipango miji na vijiji wa kanda ya ziwa atakayehusika na kuidhinisha
michoro ya mipango miji.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: