ads

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ustawi, haki za binadamu na uwezeshaji wa watoto wa kike Bilioni 1.1 ulimwenguni kote ni kitovu cha mafanikio ya malengo ya maendeleo endelevu, SDG's.


Ban amesema hayo katika ujumbe wake wa siku ya mtoto wa kike hii jana, maudhui yakiwa ni maendeleo ya mtoto wa kike ni maendeleo ya SDGs, kipi muhimu kwa mtoto wa kike.

Amesema Umoja wa Mataifa umeazimia kumaliza ubaguzi na ghasia dhidi ya mtoto wa kike, sambamba na mila potofu kama vile ndoa katika umri mdogo.

Kwa mantiki hiyo amesema ahadi imeshatolewa hakuna mtu atakayeachwa nyuma kwenye malengo hayo, wakati huu ambapo mara nyingi vijijini na hata kwenye kambi za wakimbizi watoto wa kike husahaulika.

Amesema kuwekeza kwa mtoto wa kike ni jambo la msingi kufanya na bora vile vile, hivyo ametaka kila mtu kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha watoto wote wa kike wanajumuishwa kwani kila mtoto wa kike ana umuhimu.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: