Kansela wa
Ujerumani, Angela Merkel amezindua jengo jipya la makao makuu ya Umoja
wa Afrika (AU) ambalo limepewa jina la Baba wa Taifa la Tanzania, Julius
Nyerere.
Kuzinduliwa
kwa jengo hilo jijini Adis Abba Ethiopia na Kansela Angela ambaye yuko
barani Afrika kwa ziara yake ya kikazi, kunafuatia mkakati ulionzishwa
na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe wakati akiwa mwenyekiti wa umoja huo
akisisitiza haja ya kuenzi mchango uliotolewa na Mwalimu Nyerere kwa
nchi za Afrika.
Akizungumza
kwenye mkutano wa AU miaka michache iliyopita, Rais Mugabe alimsifu
Nyerere kama mwanamapinduzi wa kweli wa Afrika aliyesaulika kuenziwa.
Aliutaka AU kutambua mchango wa Nyerere wakati wa uhai wake kwa kujenga jengo maalumu.
Kuzinduliwa kwa jengo hilo, kunakuwa ni mara ya kwanza kwa makao makuu ya umoja huo kutambua mchango wa waasisi wa Afrika.
Jengo hilo ambalo jina lake kamili ni Jengo la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili wa Ujerumani.
Litakuwa
makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU na kutumiwa na maofisa wa
kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani na kuratibu juhudi za
kulinda amani za AU.
Ujenzi wa jengo hilo ambalo linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu Euro 27 milioni.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: