RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed
Shein amelisisitiza Bunge la Jumuiya ya Afika Mashariki (EALA) kuweka
mikakati imara katika kukuza sekta ya utalii kwa nchi za jumuiya hiyo
kwani idadi ya watalii wanaoingia kwenye eneo hilo hailingani na vivutio
viliopo.
Dk Shein aliyasema hayo jana kwenye Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi,
Chukwani Mjini Zanzibar, wakati akizindua Mkutano wa Pili wa Kikao cha
Tano cha Bunge la Tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) unaofanyika
Zanzibar.
Alisema kuwa pamoja na kwamba eneo hilo la nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki lina vivutio vingi vya utalii, idadi ya watalii wasiozidi
milioni 5 wanaoingia katika eneo hilo kutoka nchi za nje ni ndogo
ikilinganishwa na watalii bilioni moja wanaosafiri kwa mwaka duniani
kote.
Dk Shein aliongeza kuwa kiasi hicho cha watalii hakilingani na
umaarufu pamoja na vivutio vilivyopo katika eneo hilo la Nchi za Jumuiya
ya Afrika ya Mashariki na kueleza matumaini yake kwamba idadi hiyo
inaweza kuongezeka iwapo juhudi za makusudi zitachukuliwa.
“Jumla ya watalii waliotembelea Zanzibar mwaka 2014 walikuwa 311,801
ambapo lengo letu ni kufikia watalii 500,000 mwaka 2020”, alisema Dk
Shein.
Aidha, Dk Shein alitumia fursa hiyo kueleza miswada inayotarajiwa
kujadiliwa katika kikao cha Bunge hilo ikiwa ni pamoja kuweka sheria
kali zitakazopiga marufuku biashara haramu ya kusafirisha binadamu
ambayo ni uhalifu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: