Kamishna Mkuu wa
Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al-Hussein
ametahadharisha kwamba, iwapo Donald Trump, mgombea wa Chama cha
Republican atashinda katika uchaguzi ujao wa rais nchini Marekani, jambo
hilo litakuwa hatari kubwa kwa dunia nzima.
Al-Hussein
amesema kwa kutilia maanani kauli zinazotolewa na Trump, kuchaguliwa
kwa mgombea huyo itakuwa hatari katika mtazamo wa kimataifa.
Kamishna
huyo amesema kauli zinazotolewa na Trump kuhusu baadhi ya matabaka ya
watu na kuidhinisha mateso kwa ajili ya kukusanya taarifa za kipelelezi
ni vitu vinavyoumiza na kusababisha wasiwasi.
Trump
amekuwa akisisitiza kuwa, ni sahihi kutumia mateso na unyanyasaji dhidi
ya watu wanaodhaniwa kuhusika na vitendo vya ugaidi wakati wa
kuwasaili.
Mgombea
huyo pia amekuwa akitoa matamshi ya kibaguzi na kichochezi dhidi ya
Waislamu na ametoa wito wa kutumiwa mbinu za manazi wa Ujerumani wakati
wa utawala wa dikteta wa zamani wa nchi hiyo Adolph Hitler, dhidi ya
Waislamu nchini Marekani.
Uchaguzi
wa Rais wa Marekani utafanyika Novemba 8 huku wagombea wakitarajiwa
kukutana katika mdahalo wa mwisho utakaofanyika mwezi huu.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: