MEYA wa zamani wa jiji la Dar es Salaam, Dk.
Didas Masaburi, aliyefariki dunia juzi usiku katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), ameacha watoto 20.
Msemaji wa familia hiyo, ambaye pia ni kaka wa marehemu, Otieno
Igogo, aliwaambia waandishi wa habari waliofika msibani Chanika, nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana kuwa mazishi yatafanyika Jumatatu.
Alisema mazishi yatafanyika eneo la Chanika kilipo Chuo cha Ununuzi
na Ugavi (IPS), ambacho ni moja ya mali za marehemu kwa kuwa mwenyewe
aliagiza azikwe kwenye eneo hilo.
Alisema marehemu enzi za uhai wake aliusia azikwe kwenye eneo hilo la
chuo kwa kuwa ndipo alipoanzia maisha na watatimiza wosia huo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: