SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema halitambui mabadiliko ya
uendeshwaji wa Klabu ya Yanga na wameuandikia uongozi wa Yanga barua
wakitaka nakala ya mkataba wa ukodishwaji wa klabu hiyo kwa miaka kumi
kwa mwekezaji anayetambulishwa kama Yanga Yetu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho hilo
Karume, Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa
alisema, TFF imekuwa ikipokea barua kutoka kwa wadau mbalimbali wa Yanga
wakihoji taratibu au hatua zinazoendelea katika mfumo wa umiliki na
uendeshwaji wa timu hiyo.
Kauli hiyo ya TFF imekuja siku chache baada ya kutolewa taarifa na
uongozi wa Yanga kwamba Bodi ya Wadhamini ya klabu hiyo imeridhia
kuikodisha kwa Kampuni ya Yanga Yetu kwa miaka kumi.
Uamuzi wa kukodisha klabu hiyo ulifikiwa na wanachama wa Yanga katika
mkutano wa dharura ulioitishwa na Mwenyekiti wake Yusuf Manji Agosti
mwaka huu, ambapo alisema ataikodisha nembo na klabu kisha baada ya
miaka kumi atairudisha.
Alhamisi iliyopita vyombo mbalimbali vya habari vilikuwa na taarifa
kuhusu muhtasari wa mkataba wa Yanga kukodishwa na Kampuni ya Yanga Yetu
Limited.
“Simba na Yanga wamekuja na mabadiliko ya kutaka kubadili mfumo wa
uendeshaji na tukaziandikia barua kutaka kukutana nazo kutaka kujua
uhalisia na Simba walikubali, lakini Yanga Kaimu Katibu Mkuu wao
(Deusdedit Baraka) alitujibu tuwasiliane na wajumbe wa Baraza la
Udhamini ndiyo wenye majibu juu ya mchakato wa ukodishwaji,” alisema
Mwesigwa.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: