BAADHI ya waathirika wa tetemeko la ardhi Manispaa ya Bukoba, wamesema kwa sasa hawahitaji msaada wa biskuti na maji.
Badala yake wamesema wanahitaji msaada wa kuwawezesha kujenga na kukarabati nyumba zao ili wapate mahali pa kulala na familia zao.
Wametoa kauli hiyo ikiwa ni siku 31 tangu lilipotokea tetemeko la
ardhi mkoani Kagera. Wakizungumza katika mkutano wa majumuisho ya ziara
ya Meya wa Manispaa ya Bukoba, Chifu Kalumuna, waathirika hao walisema
kuwa kamati ya maafa imekuwa ikipita mitaani na kuwagawia baadhi ya
waathirika maji, biskuti, mchele, unga, vyandarua na majani ya chai na
kusahau kuwa vitu hivyo siyo kipaumbele kwao kwa sasa kulingana na maafa
yaliyowapata.
Mmoja wa wakazi hao, Jacqueline Focus, mkazi wa Migera Manispaa ya
Bukoba, alisema serikali iwapelekee vifaa vya ujenzi na kuliagiza Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuingia mitaani na kuwasaidia
wananchi kurejesha majengo yao katika hali ya kawaida ili wapate sehemu
za kulala na kuepuka kunyeshewa mvua zinazoendelea kunyesha hasa nyakati
za usiku.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: