MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amis Tambwe amesema siri ya kuendelea kutikisa
nyavu katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara bila kushuka, ni kwa
vile amekuwa hasikilizi maneno ya mashabiki uwanjani.
Alisema mchezaji yeyote kama anahitaji kufanikiwa na kufanya vizuri
katika ligi hiyo hapa nchini hana budi kuziba masikio ya mashabiki na
kufanya kile ambacho kimemleta katika timu vinginevyo ni rahisi kupotea.
Tambwe hivi karibuni aliifungia bao timu yake katika mchezo dhidi ya
Simba, ingawa inadaiwa kabla ya kufunga aliushika kwa mkono mpira huo.
mchezaji huyo wa zamani wa Simba, alisema
anawajua mashabiki wengi wa soka wamekuwa ni wazungumzaji, na kwamba
kama angekuwa anawafuatisha angekuwa ameshuka kiwango.
“Siku zote ukitaka kufanikiwa katika Ligi ya Tanzania ni lazima
upambane kweli na kuacha kusikiliza maneno ya mashabiki, kwani
ukiwafuatisha utaanguka na kupotea kabisa,” alisema.
Tambwe tangu kujiunga na Simba msimu wa mwaka 2013 na msimu uliopita
Yanga, amekuwa akizidi kuonesha ubora wake katika kufumania nyavu huku
msimu uliopita akiibuka kuwa mfungaji bora.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: