ads

Wanawake wamekuwa wakitajwa kuwa tegemezi katika familia kwa kuwategemea wanaume pekee, lakini Serikali ya Awamu ya tano yenye sera ya Hapa Kazi Tu, chini ya Rais Magufuli imeendelea kuhamasisha ufanyaji kazi kwa watu wote nchini, ambapo viongozi mbalimbali wameendelea kuunga Mkono jitihada hizo.

Mmoja wa Viongozi wanaounga jitihada hizo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ambapo wakati akizindua kikundi cha Vikoba cha Magereza (Magereza Vikoba Group) ameahidi kuwasaidia mtaji kupitia ile ahadi ya Rais Mgufuli ya Milioni 50 kila mtaa na kuzungumza na baadhi ya Taasisi za kifedha kuona ni namna gani wanaweza kuwasaidia ili waweze kuinua mitaji yao na kujiendeleza kiuchumi.

Vile vile kuhusu changamoto ya eneo inayoikabili kikundi hicho Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemuagiza Diwani wa kata hiyo ya Ukonga Juma Mwaipopo kuwa pale baraza la madiwani litakapoanza kupima viwanja litoe kipaumbele kwa kikundi hicho na kukipatia eneowatakalo endesha shughuli zao, na kuahidi serikali itaendelea kuwaunga mkono na kuwashawishi wengine kujiunga na Vikoba.

Pia amewashauri wanachama wa Vikoba kujiwekea mpango wa kurejesha pesa wanazokopa au kuzungumza na walimu kwa maelezo zaidi ili kuepuka kunyang'anywa vitu vyao, Pia amewataka wanaume kuwaunga mkono wake zao wanaojihusisha na masuala ya Vikoba na kuacha Wivu usio na tija kwa kuwakataza, kwani Vikoba vinajenga uchumi wa familia, Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya huyo amechangia kiasi cha shilinig laki 7, kwa lengo la kuwaunga Mkono na kuwataka wadau mbalimbali kujitokeza.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: