BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za
Usafiri wa Nchikavu na Majini (Sumatra-CCC), limeitaka serikali
kusitisha usafiri wa bodaboda na bajaji, hadi mtaala wa kuwafundisha
madereva wa vyombo hivyo utakapotungwa na kuanza kufundishwa.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk. Oscar Kikoyo, alitoa kauli hiyo
jijini Dar es Salaam jana, wakati wa mashindano ya vilabu vya wanafunzi
wa Sumatra-CCC vilivyokuwa vikichuana kuonyesha umahiri wa sheria za
barabarani.
Dk. Kikoyo alisema wakati serikali ikiruhusu bodaboda na bajaji
kufanya biashara, ilikuwa haijajiandaa kuwa na mfumo wa kutoa huduma
hiyo.
“Hapakuwa na mtaala wa kuwafundisha, kwa hiyo mtu akitaka kuendesha
bodaboda anajifunzia mtaani mwenyewe siku moja au mbili, akijiona
ameweza anaingia barabarani kubeba abiria.
"Kwa hali ilivyo hivi sasa ajali ni nyingi watu wanapoteza maisha
tunaiomba serikali isimamishe kwanza utoaji wa huduma kwa vyombo hivi
ili tufanye maandalizi ya kina kuhusu mfumo wa utoaji mafunzo kwao,"
alisema.
Alieleza kuwa hiyo ni changamoto kubwa ambayo imesababisha
watanzania wengi kila siku kupoteza maisha kutokana na ajali
zinazosababishwa na kundi hilo.
“Vifo hivi sio tu vinatokea kwa abiria wanaowapandisha kwenye vyombo hivi, pia na wenyewe wamekuwa wakipoteza maisha,” alisema.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: