Miss Tanzania 2016,
Diana Edward ametangaza vipaumbe vyake kuwa ni kupinga ukeketaji, mila
potofu na ndoa za utotoni hasa kwenye jamii za Kimasai na nyinginezo.
Mrembo
huyo wa Kinondoni, Diana alitwaa taji la Miss Tanzania 2016, usiku wa
kuamkia Jumapili kwenye Ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.
Diana
alinyakua taji hilo na kujitwalia gari aina ya Toyota IST na kitita cha
Sh4 milioni baada ya kuwashinda warembo wenzake 29 kutoka mikoa
mbalimbali nchini waliokuwa wakichuana kuwania taji hilo.
Akizungumza
baada ya kutwaa taji hilo, Diana alisema haikuwa kazi rahisi kwani
ushindani ulikuwa mkali ni mapenzi ya Mungu kumpa nafasi hiyo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: