WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu
Nchemba, ameshangazwa na kitendo cha wananchi kukimbia na kujifungia
ndani vikundi vya kihalifu kama ‘panya road’ vinapofika kwenye mitaa
yao.
Kutokana na hali hiyo, amesema anashangazwa kwa sababu vikundi hivyo
vinaundwa na watoto wadogo wenye silaha za jadi ambazo wananchi wote
wanazo, hivyo wanaweza kuwakabili.
Nchemba ambaye anasimamia jeshi la polisi lenye dhamana ya kulinda
usalama wa raia na mali zao, alisema kitendo cha wananchi kukimbia
vijana hao halikubaliki kwa kuwa polisi hawawezi kuwa kwenye kila mtaa
kwa Wichita mmoja, hivyo ni lazima wananchi washiriki ulinzi.
“Haiwezekani mkasema ‘panya road’ wamekuja kwenye mtaa wapo wanne,
watano au 10 halafu wakanyamazisha mtaa mzima. Hii haiwezekani chamber
hawa wote wamekuja, wengine hawana hata silaha, wamekuja tu na vinanii
hivi vya jadi (silaha) ambazo na sisi tunazo halafu wananyamazisha mtaa
mzima. Hii sii lazima kusema tusubiri polisi, lazima tupambane
kuhakikisha hatuachi wahalifu kutawala maeneo yetu.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: