Spika wa Bunge mstaafu, Samuel Sitta amerejea nchini kutoka Ujerumani alikokwenda kwa ajili ya matibabu ya miguu.
Septemba mwaka huu, Sitta alikwenda nchini humo baada ya kusumbuliwa na tatizo hilo.
Mmoja
wa wanafamilia wa mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri wa wizara
mbalimbali serikalini, alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa hali
yake inaendelea vizuri.
Hata hivyo mimi siyo msemaji wa familia,” alisema mtoa habari huyo.
Alipotafutwa
mke wa Sitta, Margaret ambaye alirithi ubunge wa Urambo kutoka kwa
mumewe, alisema alikuwa benki na asingeweza kuzungumza na simu.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: