SERIKALI imetoa vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo wa 2016/2017.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,
Stella Manyanya alisema Dar es Salaam jana kuwa vigezo hivyo
vinazingatia Dira ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano,
Sera ya Elimu na Mafunzo (2014) na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Waziri huyo alisema serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu, imekuwa ikiwakopesha wanafunzi wenye sifa za kujiunga na
vyuo vya elimu ya juu nchini kugharamia masomo yao.
Alisema katika utekelezaji wa jukumu hilo, Serikali huandaa sifa na
vigezo vya utoaji mikopo kila mwaka ili kuendana na malengo na matarajio
yaliyopo katika mipango na mikakati ya kitaifa kama ilivyoainishwa
katika mipango mbalimbali. Alisema kwa kuzingatia mipango mikakati na
sera hizo, pia Mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka 2016/2017 katika
mwaka wa masomo 2016/17 umetolewa.
“Vipaumbele vya kitaifa vinayoendana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa
wa Miaka Mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na mafunzo ambayo
yatazalisha watalaamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za
kipaumbele kama vile fani za Sayansi za Tiba na Afya na fani ya Ualimu
wa Sayansi na Hisabati.
Waziri Manyanya alisema vipaumbele vingine ni Uhandisi wa Viwanda,
Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia, Sayansi Asilia na Mabadiliko ya
Tabianchi na Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
Alieleza vipaumbele vingine kuwa ni uhitaji wa waombaji hususani
wenye mahitaji maalum kama vile ulemavu na uyatima na ufaulu wa waombaji
katika maeneo ya vipaumbele na umahiri.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: