KOCHA Mholanzi Hans van der Pluijm, leo ataiongoza Yanga kuivaa Mbao FC baada ya juzi kukubali kurejea kuinoa timu hiyo.
Hatua hiyo inafuatia baada ya uongozi wa Yanga kumjibu barua yake ya
kuachia ngazi, ikimkatalia na kumtaka kuendelea na kazi kwa kuwa ana
mkataba wa miaka miwili.
Akizungumza na mwandishi wetu juzi, Pluijm alisema: "Ndiyo, nimerudi
kazini na kesho nitaendelea na majukumu yangu kwa roho safi kama kocha
mkuu".
Katika barua iliyosainiwa na Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit, Yanga
ilisema haioni sababu ya kuachana na Mholanzi huyo baada ya mafanikio
aliyoipa klabu.
Mholanzi huyo alijiuzulu mapema wiki hii baada ya kukerwa na uongozi
wa klabu kuleta kocha mpya, Mzambia George Lwandamina bila kumtaarifu,
akisema huko ni kumvunjia heshima.
Kocha huyo alikataa hata nafasi ya ukurugenzi wa ufundi ambayo
inasemekana Yanga ilitaka kumpa baada ya kumleta Lwandamina kuwa kocha
mkuu.
Lakini baada ya kuwaaga wachezaji siku moja kabla ya mchezo wa Ligi
Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu timu ikishinda 4-0, Waziri wa Mambo
ya Ndani, Mwigulu Nchemba aliingilia kati suala hilo.
Waziri Mwigulu ambaye inadaiwa ni shabiki wa Yanga, kwanza aliushauri
uongozi kumrudisha Pluijm na baadaye akaenda kuzungumza na kocha huyo
pia kumshauri akubali kurejea.
Baadaye akazikutanisha pande zote mbili, Pluijm na uongozi wa Yanga
katika kikao ambacho inaelezwa makubaliano yalifikiwa na kisha uongozi
wa Yanga kumuandikia barua Pluijm kumuomba arudi kazini.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: