ads

MINOFU ya samaki mkubwa aliyepatikana Kilwa Masoko mkoani Lindi imeanza kuondolewa ili mifupa yake ihifadhiwe kwenye Jumba la Utamaduni na Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya utalii.


Kiumbe huyo aliyepewa jina la ‘samaki wa ajabu’ akiwa na urefu futi 30 alipatikana kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi kisiwani Masoko wiki mbili zilizopita, akiwa amekufa.

Ofisa Uvuvi wa Wilaya ya Kilwa, Ahmadi Mkali, alisema jana katika mahojiano na Nipashe na kuongeza kuwa tangu kupatikana kwa samaki huyo serikali iliratibu ukusanyaji dawa zitakazotumika kukausha samaki huyo na tangu mwishoni mwa wiki iliyopita kazi ya kuondoa minofu ili ibaki mifupa ilianza.

Alisema baada ya kukamilika, mifupa hiyo itawekwa kwenye Makumbusho ya Taifa ili iweze kutumika kama moja ya kivutio cha watalii. 

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: