NI unyama! Mwanaume aitwaye Sadiki Andrew,
31, anatafutwa kwa udi na uvumba na Jeshi Polisi mkoani Tanga kwa tuhuma
za kumuua kwa kumchoma kisu shingoni mkewe Tabu Siasoni, 28.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, aliiambia
Nipashe kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi usiku katika kijiji cha
Ngarani B, Kata ya Kwakifua wilayani Muheza mkoani humo.
Akisimulia zaidi tukio hilo, Kamanda Wakulyamba alisema kuwa kabla ya
kufanya unyama huo na kisha, kukimbilia kusikojulikana, mtuhumiwa
alimsubiri mkewe Tabu apande kitandani, alale na kisha ndipo
alipomkatishia uhai wake kwa kumchoma kisu shingoni.
“Alimchoma kisu wakati akiwa amelala… baada ya kufanya mauaji hayo
mtuhumiwa alikimbilia kusikojulikana. Hadi sasa bado anatafutwa,”
alisema Kamanda Wakulyamba.
Aidha, Kamanda huyo alisema kuwa uchunguzi kuhusiana na tukio hilo
unaendelea, huku taarifa za awali zikidai kuwa chanzo cha mwanume huyo
kufikia uamuzi wa kinyama wa kumuua mkewe ni wivu wa kimapenzi. Hata
hivyo, Kamanda hakufafanua zaidi juu ya suala hilo kwa maelezo kuwa bado
uchunguzi wake unaendelea.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: