KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amesema kikosi chake kimerudi
katika kiwango chake na sasa ni mwendo wa ushindi katika mechi zake
zilizobaki.
Yanga ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika
mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru.
Mabao ya Yanga katika mechi hiyo yalifungwa na Obrey Chirwa, Simon
Msuva na Donald Ngoma na la Mtibwa likifungwa na Haruna Chanongo. Huo ni
ushindi wa kwanza kwa Yanga baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya
Stand United na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba katika mechi
zilizopita.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Pluijm alisema kiwango walichoonesha
wachezaji wake kama wataendelea nacho ni wazi kuwa wataikaribia Simba
inayoongoza kileleni.
“Ushindi huu mnono unaonesha kuwa tumerudi ni lazima tuendelee
kujiandaa asilimia 100 kwa kila mchezo wetu kuendeleza ushindi, lengo
letu ni kuikaribia Simba kileleni na kuwa rahisi kutetea taji letu,”
alisema.
Alisema kikosi chake kilicheza vizuri na kwa ushirikiano uliowezesha kutumia vyema nafasi walizopata katika kufunga.
Kuhusu Chirwa kufunga kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo
msimu huu, Pluijm alisema siri ya mafanikio ni kwa sababu alimuandaa
kisaikolojia na kumhimiza kucheza kwa kujiamini. “Nilimuandaa Chirwa na
kumhimiza kujiamini anapokuwa uwanjani na hilo limefanikiwa kwake,”
alisema.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: