Mshambuliaji aliyewahi kutamba na klabu za Arsenal na Real Madrid,
Emmanuel Adebayor, amemshangaa beki wa kati wa Yanga, Vincent Bossou,
akidai kiwango alichonacho beki huyo alitakiwa awe anachezea timu kubwa
barani Ulaya.
Adebayor, ambaye ni nahodha wa Timu ya Taifa ya Togo, amekoshwa na
kiwango cha beki huyo ambacho amekionyesha katika michezo kadhaa timu
hiyo yaTaifa ikicheza na timu nyingine.
Bossou alisema Adebayor amemhakikishia kuwa atafanya kila namna ili
kumtafutia sehemu ya kwenda kucheza huko Ulaya, ambako ndiko kwenye
hadhi yake.
“Yule ni kama kaka yangu, kwani kwenye timu ya Taifa ni nahodha,
ameniambia uwezo wangu ni mkubwa na kwamba atatafuta timu ambayo naweza
kuchezea barani Ulaya,” alisema.
Akizungumzia hatua hiyo ya Adebayor ya kutaka kumpeleka Ulaya na
kuachana na Yanga, alisema yeye anachohitaji ni changamoto mpya na
kwamba dili hilo likitiki atawaaga Yanga, kwani wameishi kwa furaha na
upendo.
“Kama atafanikiwa kunitafutia timu wala sitakataa kwenda, kwani kila
mchezaji katika Bara hili la Afrika anatamani kwenda kucheza Ulaya,
nadhani hata Yanga hawawezi kunikatalia, kwani nimeishi nao vizuri na
wangependa mafanikio yangu,” alisema.
Bossou alionyesha uwezo mkubwa na kuisaidia timu yake katika kuwania
kufuzu michuano ya fainali za Afrika dhidi ya Djibout, akifunga mabao
mawili kwenye ushindi wa mabao 5-0.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: