MKAZI wa Kilindi mkoani Tanga, Angela Basso
ametembea kwa wiki tatu hadi mkoani Dodoma, akiwa na watoto wake wawili,
kumwona Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ili kumwelezea shida zake.
Basso akiwa na watoto wake, Happy (7) na Janeth (9), amesema amefika
hapa kumwona Waziri Mkuu ili amsaidie kurejeshewa ekari 30 za mashamba
alizonyang’anywa.
Akizungumza jana mjini hapa, mwanamke huyo alisema aliporwa mashamba
hayo na kuchomewa nyumba yake katika Kijiji cha Kwendigole na wanaume
wawili, waliojitokeza kwa nyakati tofauti wakidai ni maeneo yao.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: