Hatimaye nyasi
bandia na vifaa vingine kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Nyamagana
jijini Mwanza vimewasili huku ujenzi huo ukitarajia kuanza rasmi leo,
Jumatatu.
Mwenyekiti
wa Chama Soka cha Mkoa wa Mwanza (MZFA), Jackson Songora alithibitisha
kuwasili kwa makontena mawili yenye vifaa hivyo vilivyowasili juzi,
Jumamosi.
Songora alisema kuwa
vifaa vilivyowasili ni pamoja na nyasi bandia, magoli makubwa na madogo,
gundi, trekta (kifaa cha kusafishia uwanja), nyavu na uzio.
Alisema
kuwa tayari mkandarasi amemthibitishia ujenzi kuanza rasmi Jumatatu na
kwamba anaamini ujenzi huo utakamilika kwa muda mwafaka.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: