Waziri
Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema mtu yeyote aliyepo upinzani
anatakiwa kuwa mvumilivu kwa sababu katika upande huo hakuna ‘mteremko’.
Kiongozi
huyo ambaye kwa sasa yupo Chadema amesema kuwa katika chama cha
upinzani ni kazi kubwa inayohitaji moyo wa uvumilivu kuliko mtu aliyepo
CCM.
Sumaye,
ambaye aliweka rekodi ya kushikilia nafasi ya Waziri Mkuu kwa kipindi
cha miaka 10 wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, alihamia upinzani
wakati wa harakati za Uchaguzi Mkuu na kuwa mmoja wa wasemaji wakuu wa
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakati wa kampeni.
Akizungumza
wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya Chadema wilayani
Mkuranga, Sumaye amesema dola haipatikani kirahisi na kwamba inahitaji
moyo wa kujitoa miongoni mwa wanachama na viongozi wao.
Tangu
alipojiunga na upinzani, Sumaye amekabiliwa na misukosuko kadhaa
ikiwamo kuzuiwa kuhudhuria mahafali ya umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu
mkoani Dodoma Januari mwaka huu, kitendo kilichomfanya alalamikie
watawala na kuonya kuwa kuwazuia wananchi kukusanyika kunaweza
kusababisha madhara.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: