NDEGE mpya ya Bombardier Dash 8- Q400, iliyonunuliwa hivi karibuni
imetua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma ikiwa ni ukaguzi na majaribio ya
mwisho kabla haijaanza kubeba abiria. Ndege hiyo ni kati ya mbili
zilizonunuliwa na serikali na kukodishwa ATCL.
Akizungumza muda mfupi baada ya kutua uwanjani hapo jana Mhandisi wa
Ndege wa ATCL, John Chaggu amesema baada ya safari hiyo ndege hiyo
itakuwa tayari kubeba abiria.
Amesema, katika majaribio hayo alikuwa na wakaguzi wawili wa ndege kutoka Canada wa kampuni iliyotengeneza ndege hiyo.
Chaggu amesema, safari yao kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma iliwachukua saa mbili angani.
Ilitua Kigoma saa 11:00 jioni na kuondoka saa 12:18 jioni .
Ndege hiyo ilitarajiwa kuendelea na safari ya ukaguzi kwa kwenda
kutua Uwanja wa Ndege wa Mwanza na baadaye kurudi Dar es Salaam.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: