MZUNGUKO wa
fedha katika uchumi wa Tanzania, umeporomoka kwa kasi katika kipindi kifupi
tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano na kuathiri ukuaji
uchumi karibu katika kila sekta.
Ripoti ya
kila mwezi ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliyotolewa hivi karibuni, ilieleza
kuwa mzunguko huo wa fedha, ambao huchangia kujenga uwezo wa ununuzi katika
uchumi, umefikia kiwango ambacho hakijawahi kutokea tangu mwaka 2012.
Kwa mujibu
wa ripoti hiyo, Desemba mwaka jana, mzunguko huo kwa maana ya noti na sarafu
mikononi mwa watu na kwenye akaunti za watu benki, ulikuwa asilimia 18.8 lakini
uliporomoka na kufikia asilimia 6.7 Julai.
Hali hiyo
ilitajwa na ripoti hiyo ya Agosti, kuwa imechangiwa pamoja na mambo mengine, na
hatua ya benki za biashara kupunguza utoaji mikopo kwa karibu kila sekta muhimu
ya uchumi, kutokana na sekta hizo kushindwa kurejesha mikopo.
Sekta
zilizoathirika
BoT imekiri
kuwa utoaji mikopo katika sekta binafsi ambayo ndiyo injini ya uchumi, umeshuka
kutoka asilimia 23.5 Julai mwaka jana hadi asilimia 15.2 Julai mwaka huu.
Hali mbaya
zaidi kwa mujibu wa ripoti hiyo, imeonekana katika sekta za ujenzi, uzalishaji viwandani
na hoteli na migahawa.
Katika
ujenzi, BoT ilionesha kuwa Julai mwaka jana mikopo iliyotolewa kwenda sekta
hiyo ilikuwa asilimia 22.9 ya mikopo yote, lakini Julai sekta hiyo iliambulia chini
ya asilimia sifuri ya mikopo yote kwa kupata asilimia -4.
Sekta ya
uzalishaji viwandani, BoT ilieleza kuwa mikopo imeshuka kutoka asilimia 30.7
Julai mwaka jana hadi chini ya asilimia sifuri, yaani asilimia -0.7 Julai mwaka
huu; huku sekta ya hoteli na migahahawa utoaji mikopo ukitoka asilimia 13.6
Julai mwaka jana mpaka asilimia -0.4 Julai mwaka huu.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: