NYOTA wa Yanga, Simon Msuva, amesema ni mapema mno kuuzungumzia ubingwa, kwani Ligi Kuu ya Tanzania Bara bado mbichi.
Msuva ambaye juzi alifikisha mabao 50 tangu ajiunge na
Yanga mwaka 201, alisema angalau baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi
Kuu unaweza kuanza kuuzungumzia ubingwa.
“Ni mapema pia, ila unaweza kuanza kupata taswira fulani ya mbio za ubingwa kwamba msimu huu nani na nani wanachuana,”alisema Msuva.
Alisema mahasimu wao, Simba kwa sasa wanaongoza kwa pointi sita zaidi yao, lakini wamecheza mechi moja zaidi na hiyo inamaanisha hakuna tofauti kubwa kati yao na vinara hao.
“Ligi bado mbichi sana, ngoja tucheze kwanza angalau tumalize mzunguko wa kwanza ndiyo tutaanza kupata picha,”alisema.
Yanga juzi iliilaza Mtibwa Sugar 3-1 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kufikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi saba, inazidiwa pointi sita na mahasimu wao wa jadi, Simba walio kileleni ingawa wamecheza mechi moja zaidi.
Msuva juzi alifunga bao lake la 50 akicheza mechi ya 164 tangu ajiunge na Yanga mwaka 2012 akitokea Moro United.
Bao hilo la Msuva lilikuwa la pili kwa Yanga baada ya Mzambia Obrey Chirwa kufunga la kwanza na baadaye Mzimbabwe, Donald Ngoma akafunga la tatu.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: