Kutokana na maombi ya wasomaji wengi wa mtandao huu,kuomba uwepo wa makala za ujasiriamali mdogomdogo na wengine wakiomba uwepo wa makala za mapishi,Swahiba Media leo hii inakuletea makala hii fupi ya namna bora ya kupika maandazi.
Maandazi kama ijulikanavyo ni moja ya kitafunwa bora kabisa wakati wa asubuhi na watu wengi hupendelea kula ,hii ni kutokana na ladha yake tamu na nzuri ambayo haikinaishi,sasa leo chukua nafasi hii kujifunza juu ya kupika maandazi kuanzia hatua ya kwanza hadi mwisho
MAHITAJI
1.Unga wa ngano nusu
2.Sukari glasi ndogo nusu(1 kama mpenzi wa sukari)
3.Chumvi robo kijiko cha chai
4.Hiliki punje 10
5.Custard kijiko kimoja cha chakula
6.Samli kijiko 1 cha chakula
7.Tui la nazi glasi ndogo 2
8.Hamira vijiko 2 vya chakula
9.Baking powder kijiko 1 cha chakula
10.Mafuta ya kupikia nusu lita
MAANDALIZI 1.Chekecha unga kwa kutumia chungio kwenye chombo utacho kandia unga wako.
MAANDALIZI 1.Chekecha unga kwa kutumia chungio kwenye chombo utacho kandia unga wako.
2.Chukua kikombe weka hamira,sukari vijiko 2,unga vijiko 2 na iache kwa dakika 5 mpaka ifure.
3.Chukua unga ulio uweka kwenye chombo chako,weka baking powder,chumvi,sukari,hiliki na custard kisha changanya vizuri.
4.Chukua hamira ilio umuka changanya na unga wako kisha weka na tui lako kidogo kidogo na uanze kuukanda.
5.Kanda unga kwa dakika 10 mpaka uwe mlaini kisha uache kwa dakika 5.
5.Weka samli unga wako na uendelee kuukanda na kisha uweke kwenye
container na uufunike usipitishe hewa uache tena kwa dakika 10.
6.Ukiumuka kata madonge na uyasukume kwa kutumia unga mkavu upate
duara kubwa kama chapati ila isiwe nene sana wala nyembamba sana,kisha
kata maandazi yako kwa shape ya pembe tatu.
7.Yaache maandazi yako yaumuke kwa dakika zisizo pungua 10.
JINSI YA KUPIKA 1.Weka mafuta kwenye karai yaache yapate moto kiasi kisha weka maandazi yako.
JINSI YA KUPIKA 1.Weka mafuta kwenye karai yaache yapate moto kiasi kisha weka maandazi yako.
2.Hakikisha maandazi hayawi mengi ili yaachane uweze kuyageuza kwa uzuri zaidi.
3.Ili andazi liumuke wakati wa kukaanga basi fanya kama una limwagia
mafuta juu kwa kutumia mwiko(mshebeki,jaro) wako,halafu ndio uligeuze
baada ya kuumuka.
4.Andazi likiiva epua weka kwenye chujio au tissue kulichuja mafuta.
5.Likipoa tayari kwa kula na mchuzi,samaki,chai,njugu mawe,maharage n.k.
Angalizo:Note:
1. Ili andazi liwe zuri na laini hakikisha unakanda mpaka unga unakua laini sana.
Angalizo:Note:
1. Ili andazi liwe zuri na laini hakikisha unakanda mpaka unga unakua laini sana.
2.Upe mda unga wa kurelax(kutulia) ili ulainike zaidi
3.Acha maandazi yaumuke vizuri ndio uchome
4.Ukitaka andazi liwe na nyama ndani usisukume lichapati jembamba wakati wa kukata shape yako na lisiumuke sana.
5.Na ukitaka lisiwe na nyama ndani sukuma lichapati la wastani wakati wa kukata shape yako na acha liumuke sana.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: