MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameshauri Kiswahili
kitumike kufundishia elimu ya sekondari ili kuwasaidia wanafunzi kujua
lugha yao ya Taifa.
Meya Isaya alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam juzi, wakati wa
kumbukumbu ya Meya wa kwanza Mwafrika, Kaluta Amri Abeid iliyofanyika
nyumbani kwake Magomeni.
Alisema kwamba Taifa limezembea kuitumia lugha ya Taifa na badala
yake kutumia Kiingereza jambo ambalo Meya Mwita, anaona ni kupoteza sifa
ya Taifa.
Alifafanua kwamba Taifa bado lina changamoto kubwa ya lugha ya Taifa
kutokana na kukosekana kwa misingi ya kuwasaidia wanafunzi jambo ambalo
linafanya kuwepo kwa ugumu wa kutambua lugha na hivyo kama ingetumika
lugha moja ingekuwa ni njia moja wapo ya kulitangaza taifa la Tanzania.
“Ukienda China utakuta wanazungumza Kichina, na hata kwenye mikutano
ambayo wanafanya wanatumia lugha hiyo, na sio China tu hata nchi
nyingine pia, ila ukija Tanzania unakuta watu wanazungumza Kiingereza,
ukienda kwenye mikutano lugha ambayo inatumika ni Kiingereza, sasa Taifa
letu tunalitangazaje?” Alihoji Mwita.
Alisema hao tunaotumia lugha zao, ndio watakuja nchini na kwingine duniani kujifunza kiswahili.
“Kenya wanajifunza na sasa wapo wengine ambao wanajua na wanapenda
kutumia Kiswahili, sasa kwanini sisi tuwe watumwa na lugha za wenzetu?”
alihoji Meya huyo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: