Sakata la watumishi
hewa sasa limefikia pabaya baada ya msako wa watu wanaolipwa fedha bila
kuwapo kazini kumkumba Mbunge Makete (CCM), Profesa Norman Sigalla(pichani juu)
ambaye alikuwa mkuu wa Wilaya ya Songea.
Wadau
walishawahi kueleza kuwa msako wa watumishi hewa uliwahusu wafanyakazi
wa kariba ya chini na hivyo kuokoa fedha kidogo, lakini sakata la
Profesa Sigalla limeonyesha kuwa hata kariba ya juu serikalini
inahusika.
Profesa
Sigalla anadaiwa kupokea mshahara wa ukuu wa wilaya kwa miezi
mitano baada ya kuacha kazi hiyo wakati wa Uchaguzi Mkuu na baadaye
kuchaguliwa kuwa mbunge kwa tiketi ya CCM.
Hali hiyo imeisababishia Serikali hasara ya Sh23 milioni.
Baada
ya kuacha kazi hiyo ya kuteuliwa na Rais, inadaiwa kuwa Profesa Sigalla
aliendelea kupokea mshahara wake wa ukuu wa wilaya wa Sh4.6 milioni
kutokana na ofisa utumishi wa ofisi ya katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma
kumrudisha kwenye orodha ya malipo ya mshahara
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: