WAKATI mchakato wa kumtangaza Rais wa Kwanza wa Tanzania, Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuwa mtakatifu kupitia Kanisa Katoliki
duniani ukiendelea, maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 17 ya kifo chake
jana, yameendelea kumdhihirisha kiongozi huyo kustahili heshima hiyo ya
juu ya kidini.
Kwa mara nyingine jana, Watanzania wamekumbushwa kumuenzi Mwalimu
Nyerere kwa kurejea misingi ya Azimio la Arusha, inayokataza na kupinga
vitendo vya rushwa na kuwataka viongozi wa umma kuwatumikia wananchi kwa
utu na si maslahi binafsi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana, kwenye
kongamano la maadhimisho ya kumbukizi hiyo iliyofanyika katika Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, watoa mada tofauti walitoa mada
zinazosisitiza misingi ya Azimio la Arusha na kusema ni lazima lirejewe,
ikiwa Tanzania inataka kuendelea.
Akitoa mada kuhusu Maadili ya Viongozi, Makamu Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula alisema misingi ndani
ya Azimio hilo ni dira ya uelekeo wa nchi na kuwataka viongozi wote
kufahamu kuwa wana wajibu wa kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia misingi
hiyo na si vinginevyo.
“Hali ni tofauti na wakati wa utawala wa Baba wa Taifa. Siku hizi
viongozi wa vyama tumeharibika, tunatumia vibaya madaraka na wapiga kura
nao wamejigeuza bidhaa, wamejirahisisha na kushusha thamani yao kwa
kukubali kununuliwa kama sambusa na kipande cha kuku, hayo ni makosa
makubwa, jamii ilifika pabaya,” alisema Mangula.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: