Serikali ya Tanzania
imekataa kuridhia mpango wa matumizi ya visa ya pamoja, ambao umeanza
kutekelezwa na nchi za Uganda, Kenya na Rwanda.
Sababu
ya kuukataa ni kutoridhishwa na masuala mbalimbali likiwamo la usalama
hasa tishio la ugaidi kwenye baadhi ya nchi za Afrika Mashariki.
Mpango
huo wenye lengo kuvutia watalii wa kigeni unatekelezwa chini ya mwavuli
wa umoja wa hiari na tayari visa 4,000 zimetolewa kwa watalii hao.
Kaimu
Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji wa Mambo ya
Nje, Bernard Haule alisema Serikali haijaridhika na taratibu zizotumiwa
na nchi zilizosaini mpango huo nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC).
“Wazo
la kuja na visa ya pamoja lilitolewa na Sekretarieti ya EAC,
walilifanyia utafiti ili kubaini changamoto zinazoweza kujitokeza,”
alisema.
Kutojiunga
kwa Tanzania kwenye mpango huo kunafanya ishindwe kushiriki kongamano
la utalii lililopangwa kufanyika Novemba 7 jijini London, Uingereza
baada ya kuandaliwa na nchi hizo tatu.
“Kila
nchi itatakiwa kuwa na maofisa wake wa uhamiaji kwenye balozi za nchi
wanachama, Tanzania itajiunga pindi mapendekezo yaliyotolewa na
sekretarieti yatakapotekelezwa na Serikali kujiridhisha,” alisema.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema Tanzania
inaendelea kujitegemea katika visa za utalii, kwa kuwa bado haijajiunga
na utaratibu huo.
Kuhusu
hatua ya kutoridhia mpango huo, Waziri wa Utalii wa Kenya, Najib Balala
alisema Tanzania ina wasiwasi wa ushindani kutoka Kenya.
Alisema
nchi hizo zimedhamiria kushirikiana katika sekta ya utalii kwa
kuainisha mikakati ya pamoja itakayokuwa chachu ya kuwavutia watalii wa
kigeni.
Balala alisema kujiweka kando kwa Tanzania hakutafanya nchi hizo zishindwe kusonga mbele.
Kupitia ushirikiano huo, watalii watakaoingia katika nchi hizo watalipa ada moja itakayowawezesha kutembelea maeneo yote
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: