KWA mara nyingine tena Mahakama imetupa maombi ya kupinga matokeo ya
uchaguzi yaliyofunguliwa na David Kafulila akipinga ushindi wa Husna
Mwilima wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kigoma Kusini, safari hii
uamuzi ukitolewa na Mahakama ya Rufaa.
Katika uamuzi uliotolewa jana na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya
Rufaa chini ya uenyekiti wa Jaji Mbarouk Salim akisaidiwa na Jaji
Bernard Luanda na Jaji Richard Mziray, mahakama hiyo imetupilia mbali
rufaa hiyo ya Kafulila kwa kile ilichodai imekosa miguu ya kusimama.
Mbali ya uamuzi huo, jopo hilo la majaji wa Mahakama ya Rufaa pia
limemtaka mlalamikaji ambaye hawakuwepo mahakamani kulipa gharama za
shauri hilo la madai namba 212/2016.
Majaji hao walisema wanakubaliana na maombi ya Wakili wa Serikali
Gabriel Mallata aliyepinga shauri hilo kusikilizwa kutokana na kile
alichodai kwamba halikukidhi matakwa ya sheria.
Hii ni mara ya pili kwa Kafulila kuangushwa kisheria katika shauri
alilofungua kupinga ushindi wa mgombea wa CCM Mwilima ambaye ndiye
Mbunge halali wa Jimbo la Kigoma Kusini, mara ya kwanza ikiwa ni Mei,
mwaka huu, shauri lake lilitupwa na Jaji Ferdnand Wambali wa Mahakama
Kuu aliyesikiliza shauri mama.
Kafulila katika rufaa yake kwa Mahakama ya Rufaa alikuwa akidai kuwa
Jaji wa Mahakama Kuu aliyesikiliza shauri lake hakumtendea haki kwa
kumnyima ushindi aliostahili.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: